Tangu mwaka 2022, Fondazione Jepa-Limmat imekuwa ikishirikiana na Hospitali ya Consolata Ikonda ili kutoa huduma za upasuaji za kuokoa maisha kwa watoto wanaoishi vijijini ambako huduma za afya ni finyu.

ciao
Mnamo mwaka 2024, Dkt. Boniphace Kamushaga Tresphory, daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali yetu, alitunukiwa ufadhili kamili wa kusoma Shahada ya Uzamili ya miaka mitatu katika Upasuaji wa Watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kituo cha mafunzo kilichothibitishwa na mshirika muhimu wa College of Surgeons of East, Central and Southern Africa (COSECSA).
Mnamo mwaka 2025, Taasis hiyo iliongeza msaada wake kwa kutoa ufadhili mwingine wa miaka mitatu kwa Dkt. Ndunguru Goodluck Zenobius (Upasuaji) na Dkt. Masaba Geofrey Cosmas (Tiba ya Ndani), ambao kwa sasa ni madaktari wahitimu katika Hospitali ya Ikonda. Tunashukuru kwa ushirikiano huu unaoendelea, ambao unaendelea kuwekeza katika kizazi kijacho cha madaktari bingwa nchini Tanzania.

Dkt. Boniphace na Dkt. Calisti wakiwa kwenye chumba cha upasuaji.

Kutoka kulia: Dkt. Boniphace, Dkt. Calisti na Dkt. Goodluck Zenobius.


