Kwa zaidi ya miaka Mingi Hospitali ya Consolata imekuwa ikitegemea ufadhili wa watu wengi waliojitolea Toka bara la Ulaya ambao wamewezesha Hospitali kukua kwa kiwango Cha Juu katika huduma za Kiafya na kutoa mchango mkubwa wa kutoa mafunzo kwa Madaktari wenyeji, kuwahimiza kutafuta utaalamu wa matibabu, kwa mfano Daktari wa Mifupa, Urolojia, Matabibu Kiujumla, Magonjwa ya Uuzazi, Tiba za Ndani, Tiba za dharura na Radiolojia. Hospitali ilijitolea kikamilifu kuwawezesha Madaktari watatu katika ubobevu wao wa kitabibu. Mwaka 2022 wenyeji wetu ni Basati Masige (Tiba za Dharura), Lunginyo ilomo (Tiba za ndani), na Jonathan Mathayo (Mtaalamu wa Radiolojia).

Madaktari Bingwa katika Tanzania walipata Ufadhili katika Chuo ambacho kipo Jijini Dar Es Salaam, kwa zaidi ya kilomita 800 kutoka Ikonda, Gharama za usaili, Karo pamoja na Vitabu zinavyofikia Yuro 2,400–2,550 kwa mwaka mmoja kwa Mwanafunzi mmoja. Kwa kipindi Cha masomo Yao wenyeji wetu waliendelea Kupata kupokea malipo ya Yuro 8,000 kwa mwaka hii ilitolewa na Hospitali ili kuwezesha  Mahitaji Yao na Familia zao.

Mchango wa Yuro 3,800 itasaidia katika Karo na Makazi kwa mwanafunzi mmoja kwa mwaka , Gharama za Jumla kwa ajili ya program ya ufadhili ni Yuro 34,200 kwa miaka Mitatu, ambapo ni sawa na Yuro 11,400 kwa mwaka mmoja. Tunatoa shukran zetu za dhati kwa kujali kwako na kuonesha ushirikiano wako kwa kubeba Jukumu muhimu la kuwezesha kituo hiki muhimu cha Nchini Tanzania.